CULTURE Titi la mama Published 9 years ago Dr Munye9y ago TITI LA MAMA Titi la mama nitamu,hata likiwa la mbwa, Kiswahili naazimu,sifayo iliyofumbwa, Kwa wasiokufahamu,niimbe ilivyo kubwa, Toka kama mlizamu, funika palipozibwa, Titile mama litamu ,Jingine halishi hamu. Lugha yangu ya uchocho,hata sasa nimekua, Changu ulimi mzicho,sasa kusema najua, Ni sawa na manukato,moyoni mwangu na pua, Pori bahari na mcho,napita nikichumia, Titile mama litamu,jingine halishi hamu. TRANSLATION OF THE FIRST POEM One's mother's breast is the sweetest Canine it may be, And thou,Swahili,my mother- tonque, art still the dearest to me. My song springs forth from a welling heart, I offer thee my plea That who have not known thee, may join in hormage to thee. One's mother's breast is the sweetest, no other so satisfies. WhatsApp Facebook Twitter Email